SIRI YAFICHUKA TIMU ZA JESHI KUBORONGA

Bingwa - - UCHAMBUZI/HABARI -

NA SHARIFA MMASI

MKURUGENZI wa Michezo wa Jeshi Tanzania, Kanali Richard Mwandike, ameeleza sababu mbalimbali zinazopelekea timu za majeshi kufanya vibaya katika soka.

Akizungumza na BINGWA jana, Mwandike alisema sababu inayopelekea timu hizo kuonekana kupanda na kushuka viwango, ni kozi za mafunzo, ambazo wachezaji wengi husomea kwa nyakati tofauti tofauti.

“Timu za jeshi zinafanya vizuri sana kwenye michezo mbalimbali na mara kwa mara zinachukuwa makombe kwenye mashindano mengi yanayofanyika kila mwaka ndani na nje ya Tanzania.

“Nikizungumzia upande wa soka, timu kubwa zinazotamba kwa sasa Ligi Kuu zinaonekana kutuzidi mbinu kisoka kutokana na wachezaji wengi wa jeshi kukabiliwa na mafunzo ya mara kwa mara.

“Niweke wazi kwamba, wachezaji wa timu za jeshi upande wa soka, wana viwango vya kimataifa tofauti na mashabiki wanavyozitolea macho,” alisema Mwandike.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.