Bill Nas adai ‘degree’ moja haitoshi

Bingwa - - BURUDANI -

NA MWANDISHI WETU

ORODHA ya mastaa wa Bongo Fleva wasomi imezidi kuongezeka mara baada ya rapa, Bill Nas, juzi kupata shahada (degree) ya kwanza ya biashara katika Chuo cha Biashara (CBE), jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Papaso la Burudani, Bill Nas, alisema anawashukuru mashabiki, vyombo vya habari, Mr T Touch, TID na Mwana FA kwa kuwa nyuma yake kipindi chote alichokuwa anasoma na kufanya muziki.

“Huu si mwisho bali ni mwanzo mpya wa William na Bill Nas mwingine, naamini bado nina safari ndefu kielimu na kimuziki, lakini niombe radhi kwa vyombo vya habari maana kuna muda nilishindwa kufanya interview za hapa na pale kutokana na kubanwa na masomo, lakini hivi sasa nipo freshi,” alisema Bill Nas.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.