‘Shikamoo Yesu’ yamtambulisha Mwanyamaki

Bingwa - - BURUDANI -

NA MWANDISHI WETU

MWIMBAJI wa nyimbo za Injili, Mathias Mwanyamaki, amesema licha ya kuachia audio pekee ya wimbo wake wa Shikamoo Yesu, ameanza kujipatia mashabiki kutokana na jina la hiyo kazi.

Akizungumza na Papaso la Burudani, Mathias alisema alitumia muda mrefu kubuni jina la wimbo pamoja na mashairi ambayo yatawapa shauku mashabiki wa Gospo ndani na nje ya nchi.

“Hivi sasa upo mtandaoni ni wimbo wa kumsifu Mungu ambao nimetumia miaka mitatu kuandika mashairi na kutafuta jina ambalo watu watajiuliza nimeimba nini ndani yake, nashukuru mashabiki wamenipokea vizuri na video ndani ya mwaka huu itakuwa tayari,” alisema Mwanyamaki.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.