P-Square kuupiga bei mjengo wao

Bingwa - - NOLLYWOOD - LAGOS, Nigeria

KAMA bado ulikuwa huamini kuwa Kundi la P-Square limevunjika, basi sikia hii. Mapacha waliokuwa wanaunda kundi hilo, Peter na Paul Okoye, wanaiuza nyumba yao ya kifahari ambayo mashabiki wao waliipachika jina la ‘Squareville’.

Tayari madalali wako ‘bize’ kusaka mteja wa mjengo huo wa kisasa unaopatikana katika Jimbo la Omole mjini Lagos, ambao wawili hao walikuwa wanaishi.

Huenda haijatajwa sababu ya kuiuza, wadadisi wa mambo wanahisi uamuzi huo umetokana na uhusiano mbaya uliopo kati ya ndugu hao, ambao ulisababisha Kundi la P-Square kuvunjika.

Peter na Paul walihamia kwenye jumba hilo mwaka 2010 na lilijengwa kwa gharama inayotajwa kufikia kitita cha Naira milioni 100, zaidi ya Sh milioni 600 za Tanzania.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.