Mwigizaji akaliwa kooni kisa wifi yake

Bingwa - - NOLLYWOOD - LAGOS, Nigeria

MWANADADA nayefanya vizuri kwenye soko la filamu, Annie Idibia, amejikuta kwenye wakati mgumu kutoka kwa mashabiki wake baada ya mwanadada mmoja anayetajwa kuwa wifi yake kusema anamtesa.

Licha ya kwamba bado Annie hajathibitisha kuhusika katika unyanyasaji huo, tayari mashabiki wake wameanza kumtupia vijembe kupitia mitandao ya kijamii.

Katika kipande cha video kilichosambaa kwenye mitandao ya kijamii, mrembo Doris ameelezea anavyoteswa na msanii huyo ambaye anashirikiana na mama yake mzazi.

Kwa mujibu wa Doris, sababu kubwa ya kufanyiwa visa na wawili hao ni kitendo chake cha kuomba ndoa na Wisdom Macauley, kaka wa Annie.

Taarifa zinasema Doris na Macauley wana watoto wawili na wamekuwa pamoja kwa miaka minne.

Hata hivyo, kitendo cha mwanadada huyo kuomba ndoa kimeonekana kupingwa na familia ya mwanamume huyo, wakiwamo dada na mama yake.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.