Upasuaji wa kansa wamwibua Banky W

Bingwa - - NOLLYWOOD - LAGOS, Nigeria

IKIWA ni mwezi umepita tangu alipofanyiwa upasuaji wa kansa ya ngozi, mwanamuziki Banky W, ameibuka na kuwashukuru mashabiki wake.

Staa huyo alitumia akaunti yake ya mtandao wa Twitter kutoa shukrani zake kwa Mungu na kila mmoja aliyekuwa akimtakia afya njema na kumuunga mkono.

"Nashukuru kwa upendo wote. Nimefurahi mno. Nimerudi, namshukuru Mungu.!!" aliandika.

Alhamisi ya wiki iliyopita, msanii huyo aliwashangaza mashabiki wake kupitia mitandaoni, alipoposti picha ya sehemu ya bega lake lililofanyiwa upasuaji.

Upasuaji wa mwezi uliopita ulikuwa wa tatu na ulilenga kuondoa uvimbe kwenye bega lake. Kwa mujibu wa msanii huyo, mingine ilifanyika miaka 10 iliyopita.

Mashabiki wake wajiandae na filamu yake mpya iitwayo ‘The Wedding Party’ ambayo itatoka hivi karibuni na itafuatiwa na ndoa yake na mrembo matata, Adesua Etomi, ambaye amekuwa akionekana naye mara kwa mara.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.