WATANIKOMA

Messi apania kufanya ‘mauaji’ Kombe la Dunia

Bingwa - - SPORTS EXTRA - BUENO AIRES, Argentina

KWA kile ambacho unaweza kusema ni kama amepanga kufanya makubwa wakati wa fainali za Kombe la Dunia, straika wa Argentina, Lionel Messi, amesema kwamba amepanga kufanya makubwa na ndio maana amepumzishwa katika kikosi ili zikianza zimkute yupo kwenye ubora wa hali ya juu.

Tulizungumza na Sampaoli kwamba msimu huu tumeshacheza mechi nyingi zikiwamo za Ligi ya Mabingwa, Copa del Rey...

STRAIKA wa Arsenal, Olivier Giroud, amesema kwamba hana cha kujutia kuhusu uamuzi wake wa kubaki kwenye klabu hiyo ya Ligi Kuu England.

Kauli hiyo ya Giroud imekuja baada ya mwishoni mwa msimu uliopita kuhusishwa kuitema Gunners, lakini badala yake akaamua kubaki.

Hata hivyo, msimu huu Mfaransa huyo hajawahi kucheza kwenye kikosi cha kwanza katika michuano ya Ligi Kuu England na huku akiwa amefunga bao moja katika michezo yote 10 aliyotokea benchi.

Akizungumza juzi, Giroud ambaye aliifungia timu ya taifa bao katika ushindi wa 2-0 walioupata Ijumaa katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Wales, alisema pamoja na hali hiyo bado anajisikia mwenye furaha kuitumikia klabu hiyo ya Emirates.

“Kwa sasa sijiulizi binafsi kuhusu hatima yangu,” staa huyo aliyaambia magazeti ya Uingereza.

“Najisikia mwenye furaha nikiwa Arsenal na nipo vizuri kuhusu uamuzi wangu kwa sababu vile vile naipenda. Nadhani habari baina yangu na klabu bado hazijamalizika,” aliongeza Mfaransa huyo.

Uwanja wa Ohio Stadium upo katika mji wa Columbus nchini Marekani na uwezo wake unachukua watazamaji 104,944 Uwanja huo ambao jina lake la kimichezo unafahamika kama ‘The Horseshoe’, ndio ulikuwa ukitumiwa na timu inayoshiriki Ligi Kuu ya Marekani MLS, Columbus Crew hadi mwaka 1999 ilipohamia kwenye uwanja wake.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.