MESSI APANIA KUFANYA ‘MAUAJI’ KOMBE LA DUNIA

OMOG ATUA NA ‘BEGI’ MBEYA STARS YAIBANA BENIN IKIBEBWA KWAO

Bingwa - - MBELE - BUENO AIRES, Argentina

KWA kile ambacho unaweza kusema ni kama amepanga kufanya makubwa wakati wa fainali za Kombe la Dunia, straika wa Argentina, Lionel Messi, amesema kwamba amepanga kufanya makubwa na ndio maana amepumzishwa katika kikosi ili zikianza zimkute yupo kwenye ubora wa hali ya juu.

Juzi Messi alikuwa miongoni mwa kikosi hicho cha Kocha Jorge Sampaoli, kilichopata ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Urusi, lakini atakaa pembeni katika mchezo mwingine wa kesho dhidi ya Nigeria.

Akizungumza juzi, staa huyo mwenye umri wa miaka 30 ambaye msimu huu ameshaifungia Barcelona mabao 16 katika michezo 17 aliyocheza katika mashindano yote, alisema kwamba, baada ya mikikimikiki katika mechi hizo ina maana sasa anatakiwa kupumzika.

"Tulizungumza na Sampaoli kwamba msimu huu tumeshacheza mechi nyingi zikiwamo za Ligi ya Mabingwa, Copa del Rey, La Liga na nyingine za timu ya taifa na tumesafiri sana,” alisema Messi na kuongeza:

"Nahitaji kwenda kushiriki fainali za Kombe la Dunia nikiwa katika ubora wa hali ya juu.”

Katika mchezo huo iliwachukua hadi dakika ya 86, Argentina kuifunga Urusi kwa bao lililowekwa kambani na straika, Sergio Aguero, likiwa ni la 35 kuifungia timu ya Taifa.

Bao hilo linamfanya staa huyo wa Manchester City kushika nafasi ya tatu sawa na Hernan Crespo katika orodha ya wafungaji bora wa Argentina na Messi anajisikia mwenye furaha kwa rafiki yake kufikisha rekodi hiyo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.