MBAO FC WAKALI WA FA CUP ‘WAN ANGA ZA MBEY

Bingwa - - JUMATATU SPESHO -

NA SALMA MPELI

MSIMU wa mwaka 2013/14, ulikuwa wa kwanza kwa timu ya Mbeya City ya jijini Mbeya kushiriki michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL). Mbeya City ambayo ilikuwa ikinolewa na kocha Juma Mwambusi wakati huo, ilionekana kujidhatiti vilivyo na katika msimu wake huo wa kwanza, ilimaliza ligi ikiwa nafasi ya tatu.

Msimu uliofuata, timu hiyo iliendeleza moto wake ingawa kasi yao ilionekana kupungua kidogo lakini waliweza kupambana na kufanikiwa tena kumaliza mbio za kuwania ubingwa wa VPL wakiwa kwenye nafasi ya nne.

Mbeya City ilikuwa timu pekee iliyopanda na kuonyesha changamoto kwenye ligi na hata kuziwekea ngumu timu kubwa za Simba, Yanga na Azam.

Timu hiyo haikuwa ikipoteza mechi kirahisi, hasa ilipokuwa kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Sokoine mjini Mbeya, ingawa Yanga walikuwa wa kwanza kuvunja mwiko huo.

Lakini baadaye mwenendo wa timu hiyo ulianza kubadilika na kuwa wa kusuasua. Tatizo lilianzia wapi?

Hiyo ilikuwa ni baada ya kuondoka kwa kocha wao Mwambusi ambaye alichukuliwa na kwenda kuwa kocha msaidizi kwenye klabu ya Yanga.

Mbali na kuondoka kocha wao, lakini kubwa lililowaangusha Mbeya City ni kuondoka kwa wachezaji wao tegemeo kwenye kikosi cha kwanza na kwenda kujiunga na klabu nyingine za Ligi Kuu.

Mbeya sasa imekuwa ikiishi kwa matumaini na mwenendo wake hautishi tena kama ilivyokuwa awali hali iliyofanya msimu uliopita kuponea chupuchupu kushuka daraja kabla ya kuokolewa na mechi tatu za mwisho.

Lakini sasa, hali iliyowakuta Mbeya City imeonekana kujirudia msimu huu kwa Mbao FC ya jijini Mwanza kutokana na mwenendo wake Ligi Kuu.

Mbao iliyopanda daraja msimu wa 201516 na kuanza kushiriki Ligi Kuu msimu wa 2016-17, ilikuwa mwiba mchungu kwa klabu za Simba, Yanga na Azam.

Mbao waliingia Ligi Kuu kama ambavyo walivyofanya Mbeya City na mashabiki wa soka nchini waliisifu kutokana na kuleta changamoto na mageuzi ya soka.

Ilifanikiwa ‘kuzikazia’ timu hizo ambazo zinaonekana watawala wa soka hapa nchini. Kila walipokutana na Mbao ni kama walikwaa kisiki kwani wengine waliambulia kichapo, wapo waliotoka sare na wengine kuponea chupuchupu kufungwa.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.