Nandy afurahia mapokezi Nigeria

Bingwa - - BURUDANI -

NA CHRISTOPHER MSEKENA

MKALI wa Bongo Fleva, Faustina Charles ‘Nandy’, amesema amefurahishwa na mapokezi ya hadhi ya VIP aliyoyapata juzi nchini Nigeria, wakati akihudhuria sherehe za utolewaji wa tuzo za All Africa Music (Afrima 2017).

Staa huyo wa singo ya Mahabuba, ambaye ni miongoni mwa wasanii wa Tanzania wanaowania tuzo hizo ambazo zimetolewa usiku wa kuamkia leo jijini Lagos, Nigeria, amesema mapokezi aliyopata yamefanya aone namna gani muziki wake unathaminika barani Afrika.

“Nimepokewa vizuri kutoka uwanja wa ndege mpaka hotelini, juzi pia nilitumbuiza kwenye kijiji cha Afrima na kuona namna muziki wangu unaeleweka huku Nigeria, nasubiri leo (jana) usiku ndiyo tuzo zinatolewa,” alisema Nandy.

Mbali ya Nandy wasanii wengine wanaowania tuzo za Afrima mwaka huu ni Vanessa Mdee, Ali Kiba, Diamond Platnumz, Lady Jay Dee, Feza Kessy, Darassa na Msafiri Zawose.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.