XHAKA AWAPA SOMO IRELAND KASKAZINI

Bingwa - - SPORTS EXTRA - BELFAST, Ireland Kaskazini

STAA Granit Xhaka, amekipa somo kikosi cha Ireland Kaskazini akikieleza kwamba inabidi kuachana na yaliyotokea na badala yake kigange yajayo, baada ya kuadhibiwa kwa penalti katika mazingira...

STAA Granit Xhaka, amekipa somo kikosi cha Ireland Kaskazini akikieleza kwamba inabidi kuachana na yaliyotokea na badala yake kigange yajayo, baada ya kuadhibiwa kwa penalti katika mazingira ya kutatanisha ambayo iliwapa Uswisi ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza wa kutafuta nafasi ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia uliopigwa juzi mjini Belfast.

Katika mchezo huo mwamuzi, Ovidiu Hategan, aliamuru ipigwe penalti baada ya kudai kuwa staa Corry Evans, alinawa mpira wakati akipokea pasi ya Xherdan Shaqiri, ikiwa ni dakika ya 58, licha ya picha za video kuonesha kuwa mpira huo ulimgonga mgongoni nyota huyo wa timu ya Blackburn.

Adhabu hiyo ndiyo iliyompa nafasi staa, Ricardo Rodriguez, kuipatia bao Uswisi ambalo limewafanya waende katika mchezo wa marudiano wakiwa na ushindi huo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.