Mugabe yaichapa Dar Sports

Bingwa - - HABARI -

NA VALERY KIYUNGU

KIKOSI cha Mugabe FC kimeibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Dar Sports katika mchezo wa Ligi Daraja la Tatu, Wilaya ya Ubungo uliochezwa Uwanja wa Kinesi, jijini Dar es Salaam juzi.

Katika mchezo huo, mabao ya washindi yalifungwa na Nuru Msabaha, Abuu Ramadhan aliyefunga mawili na Dargon Charles.

Msabaha alikuwa wa kwanza kuiandikia timu yake bao dakika ya tisa, kabla ya Ramadhan kuongoza la pili na la tatu dakika ya 27 na 39.

Baadaye Charles alifunga bao la nne dakika ya 78, baada ya Dar Sports kupata bao dakika ya 87 lililofungwa na George Isubu.

Katika mchezo mwingine, Sinza Boys ilifanikiwa kuondoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Makoka katika mchezo mkali uliochezwa Uwanja wa Shule ya Msingi Ukombozi, Manzese juzi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.