Redknapp: Terry ataenda Aston Villa

Bingwa - - EXTRA -

LONDON, England

KOCHA wa zamani wa Tottenham, Harry Redknapp, ametoboa siri kuwa nahodha wa zamani wa Chelsea, John Terry, aliyetangaza kustaafu soka hivi karibuni atajiunga kwenye benchi la ufundi la timu ya Aston Villa aliyocheza msimu uliopita.

Hivi karibuni kumekuwa na tetesi za mkongwe wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry, ambaye ni kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Ubelgiji anapewa nafasi kubwa kuchukua mikoba ya Steve Bruce aliyetimuliwa huku Terry akitajwa kuwa msaidizi wake.

“Usiku nilikutana na Terry tuliongea mambo mengi, nahisi atajumuishwa katika benchi la ufundi la Aston Villa, uhakika juu ya hilo ni mkubwa kwa upande wangu,” alisema Redknapp.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.