Bale aitia hofu Wales

Bingwa - - EXTRA -

CARDIFF, Wales

KOCHA wa timu ya Taifa ya Wales, Ryan Giggs, anasubiri taarifa ya majeraha ya winga wake anayekipiga Real Madrid, Gareth Bale, ambaye alishindwa kumaliza mchezo uliopita dhidi ya Alaves.

Bale amezua hofu kubwa kambini Wales ambako wanaamini atakuwa fiti kujiunga nao kabla ya mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Hispania wiki ijayo, pia alikosa mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wiki iliyopita dhidi ya CSKA Moscow.

Gigs na benchi lake la ufundi wanaamini mfungaji huyo wa muda wote wa Wales, atarejea mapema kujinoa na kikosi cha taifa hilo ikiwa hivi sasa yupo chini ya uangalizi maalumu.

“Anatamani kujumuika na sisi mazoezini, ni vizuri kuwa na nyota wenu kikosini, tunaamini atarudi mapema ni mchezaji muhimu kwetu,” alisema kiungo wa Stoke City, Joe Allen.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.