Essien amng’ata sikio Hazard

Bingwa - - EXTRA -

LONDON, England

KIUNGO wa zamani wa Chelsea, Michael Essien, amemshauri Eden Hazard kupuuzia habari zinazosema ataondoka ndani ya kikosi hicho chenye maskani yake Stamford Bridge, London.

Hivi karibuni Hazard alibainisha alikuwa na ndoto za kujiunga na Real Madrid lakini anaamini bado ana kazi ya kuifanya Chelsea kabla ya kuondoka, huku akitengewa mshahara wa pauni 300,000 kwa wiki ndani ya klabu hiyo ya England.

Essien ambaye alishinda mataji tisa kwa misimu nane aliyokuwa Chelsea, alijiunga na Real Madrid msimu wa 2012/13 chini ya Jose Mourinho ambaye hivi sasa ni kocha wa Manchester United.

“Hazard ana furaha Chelsea, tunaamini ataendelea kuwepo hapa mpaka mwishoni mwa msimu na kuongeza mkataba kwa mara nyingine.

“Kwa sasa apotezee uvumi wowote unaomhusu na kumtaja kuwa anataka kuondoka Chelsea.” Alisema Essien ambaye anaamini kila mchezaji ndani ya klabu hiyo ana furaha tangu Maurizio Sarri ajiunge nao.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.