Moyes amtetea Mourinho Man U

Bingwa - - EXTRA -

MANCHESTER, England

KOCHA wa zamani wa Manchester United, David Moyes, ametoboa siri kuwa mabosi wa kikosi hicho watampa muda zaidi Jose Mourinho ambaye anatajwa kuondoka ndani ya timu hiyo.

Moyes alifukuzwa kazi na Manchester United baada ya kuwa na kikosi hicho kwa miezi tisa akichukua nafasi ya Sir Alex Ferguson ambaye alistaafu kufundisha soka.

Kocha huyo wa zamani wa Everton aliondoshwa kikosini humo haraka baada ya klabu hiyo kushindwa kupata matokeo mazuri chini yake, lakini Moyes anaamini Mourinho atapewa muda zaidi sababu alizaliwa kuwa mshindi.

“Jambo zuri zaidi timu hiyo ilishinda mchezo dhidi ya Newcastle United, haijalishi unashinda vipi lakini alifanya hivyo kwa kucheza vizuri.

“Mourinho amepewa muda na atapewa mwingine zaidi ili kujenga timu hiyo sababu alizaliwa kuwa mshindi, alishathibitisha hilo katika klabu zake alizofundisha,” alisema Moyes.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.