Dogo wa Dortmund apagawa kuitwa England

Bingwa - - EXTRA -

LONDON, England

KINDA wa England, Jadon Sancho anayekipiga katika klabu ya Borrusia Dortmund ya Ligi Kuu Ujerumani, Bundesliga, amejumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa huku akibainisha kuwa alikuwa na mshtuko baada ya kusikia jina lake.

Sancho amekuwa katika kiwango cha juu sana ndani ya Bundesliga tangu atoke Manchester City msimu uliopita, ikiwa mpaka sasa anaongoza kwa kutoa asisti nyingi zaidi ndani ya ligi kubwa tano za Ulaya, ametoa asisti sita.

“Nilikuwa mazoezini (Borrusia Dortmund) wakati kocha ananiita katika kikosi cha England, haraka nilipiga simu kwa wazazi wangu kuwajulisha hilo, hakika walikuwa kwenye furaha sana.

“Nilishangaa sana kuitwa na kocha wa nchi yangu, umri wangu ni mdogo sana wala sikutegemea kabisa kuvaa jezi ya England hivi karibuni,” alisema Sancho.

Kocha wa England, Gareth Southgate, amemjumuisha kwa mara ya kwanza kikosini kinda huyo wa miaka 18 katika timu ya England inayotarajiwa kucheza michezo miwili ya Ligi ya Mataifa Ulaya dhidi ya Croatia na Hispania.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.