Dodoma FC kucheza mechi 4 za kirafiki

Bingwa - - HABARI - NA RAMADHAN HASSAN, DODOMA

TIMU ya Dodoma FC inatarajia kucheza michezo minne ya kirafiki kabla ya kuivaa Green Warriors katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara, utakaochezwa Oktoba 20, mwaka huu.

Akizungumza na BINGWA jana jijini hapa, Katibu wa timu hiyo, Fortunatus John, alisema michezo hiyo itawasaidia kuwajengea ufiti wachezaji wao.

John alisema timu yao inatarajia kucheza na Mtibwa Sugar katika mchezo wa kirafiki utakaochezwa leo kwenye Uwanja wa Manungu, mkoani Morogoro.

Alisema baada ya mchezo huo watacheza na Mawenzi Market kesho katika Uwanja wa Jamhuri, mkoani Morogoro.

Katibu huyo alisema timu hiyo itacheza michezo mingine miwili ya kirafiki dhidi ya African Lyon na Azam.

Alisema mchezo wao dhidi ya African Lyon utachezwa Oktoba 14 na ule wa Azam utachezwa Oktoba 15 mwaka huu, kwenye Uwanja wa Azam Complex, jijini Dar es Salaam.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.