Serengeti mabingwa Kombe la FA Mara

Bingwa - - HABARI -

NA DAMIAN MASYENENE, MWANZA

MKOA wa Mara umepata mwakilishi wa michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), maarufu Kombe la FA, ambaye ataungana na bingwa wa Ligi Daraja la Tatu ngazi ya mkoa katika droo itakayopangwa hivi karibuni.

Timu ya Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti (Hawise FC), ilinyakua ubingwa wa Kombe la FA ngazi ya Mkoa wa Mara, baada ya kuinyuka timu ya Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Hawita FC) katika mchezo wa fainali.

Hawise walishinda bao 1-0 dhidi ya Hawita katika fainali iliyopigwa juzi kwenye Uwanja wa Sokoine, mjini Serengeti, Mara.

Bao pekee kwa mabingwa hao wapya wa Kombe la FA Mkoa wa Mara lilifungwa na Steven Mapunda, katika dakika ya 14.

Akizungumza na BINGWA juzi, Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Mara (FAM), Samwel Mziba, alisema chama hicho kitaziandaa timu zitakazouwakilisha mkoa huo katika michuano hiyo ziweze kukabiliana na ushindani.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.