Kumbe Adidas wamejitoa mhanga kwa Arsenal

Bingwa - - MAKALA/HABARI -

MKURUGENZI mkuu wa kampuni ya vifaa vya michezo ya Adidas, Kasper Rorsted, amekiri kwamba timu ya Arsenal bado haina ubora wa kutosha ingawa anaamini watafanya jambo kubwa hivi karibuni.

Bosi huyo wa Adidas alisema hayo baada ya kampuni yake hiyo kukubaliana dili la kudhamini jezi za washika mitutu hao wa London mapema wiki hii, lenye thamani ya pauni milioni 300.

Alisema katika miaka mingi Arsenal imekuwa ikicheza chini ya kiwango, lakini ana imani na kikosi cha sasa cha kocha, Unai Emery, kitafanya makubwa kufuatia mwanzo wao mzuri msimu huu.

“Arsenal ni jina kubwa duniani lakini kwa miaka mingi tmu yao haijawa na kiwango cha kuridhisha. Lakini ukiwatazama kwa sasa wanaonesha matumaini mapya,” alisema.

“Wikiendi iliyopita waliwatandika Fulham mabao 5-1 halafu walicheza soka safi. Bao la Aaron Ramsey lilikuwa tamu mno. Basi tu waliburudisha wengi wakiwa na jezi zisizo sahihi!” alitamba Rorsted.

Klabu hiyo inatarajiwa kuanza kutumia jezi zitakazotengenezwa na Adidas, ambao mara ya mwisho walivaa jezi zao mwaka 1994, mara baada ya mkataba wao na kampuni ya Puma kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.