Itakuwa hatari ndani ya Songea

Bingwa - - IJUMAA SPESHO -

VUMBI la tamasha la Tigo Fiesta 2018, litaendelea kutimka leo kwenye Uwanja wa Majimaji, mjini Songea. Hili litakuwa ni onyesho la nne la tamasha hilo linaloandaliwa na Kampuni ya Clouds Media Group na kufanyika kila mwaka katika mikoa mbalimbali nchini, baada ya kuanzia Morogoro, Sumbawanga na Iringa.

Tamasha hilo ambalo linadhaminiwa na Kampuni ya Mtandao wa Mawasiliano wa Tigo na mwaka huu limepewa kaulimbiu ya ‘Vibe Kama Loteeeee!.

Wasanii mbalimbali watakaokamua kwenye onyesho hilo ni Lulu Diva, Mr Blue, Fid Q, Roma Mkatoliki na Stamina ‘Rostam’, Weusi, Chegge, Barnaba, Mesen Selekta, Foby, Zaid, Ruby na wengineo wa mjini Songea.

Katika tamasha lililofanyika mjini Iringa, wasanii waliopanda jukwaani walifanya shoo kabambe iliyokonga nyoyo za wakazi wa mji huo na maeneo ya jirani.

Akizungumza mbele ya umati wa mashabiki waliohudhuria tamasha hilo kwenye uwanja huo wa Samora, Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini, Richard Kasesela, aliipongeza kampuni ya Tigo kwa kuwapelekea burudani na fursa mbalimbali kwa wakazi wa Iringa.

“Hii ni fursa ya pekee kwa wakazi wa mji huu ambayo kampuni ya Tigo imetuletea kwa mara nyingine ndani ya mkoa huu. Ukiondoa burudani, pia wafanyabiashara wamenufaika sana ndani ya wiki nzima,” alisema Kasesela.

Pia, mkuu huyo wa wilaya alipata nafasi ya kumkabidhi zawadi ya keki msanii Chege Chigunda kwa kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwake.

Kwa upande wa burudani, wasanii wa kundi la Weusi ndio waliofunika kwenye tamasha hilo ilipopelekea mashabiki kuomba wasitoke kwenye jukwaa na kundi la Weusi walifanya hivyo hadi mwisho wa shoo kwa kuimba nyimbo zao nyingi za kuvutia zikiwemo, Madaraka, Swagire, NiCome na nyingine nyingi.

Akizungumzia tamasha la Iringa, Katibu Mkuu wa Kamati ya Maandalizi ya Tigo Fiesta 2018, Gardner G. Habash, aliwahakikishia burudani ya hali ya juu wote watakaohudhuria tamasha hilo mjini humo.

“Katika miaka ya hivi karibuni, tumetambua mchango mkubwa wa kiuchumi na kijamii unaotokana na tamasha la Tigo Fiesta. Mbali ya kutoa fursa ya kuutangaza mkoa husika, pia inaongeza idadi ya wageni na kusababisha ongezeko kubwa la fursa za biashara kwa wamiliki wa hoteli, migahawa, mama ntilie, vyombo vya usafiri kama vile bodaboda, kumbi za starehe na biashara nyingin Habash.

Kwa upande wak Huduma za Masoko William Mpinga, ali inatoa punguzo ku tiketi za tamasha la 2018 zitakazonunu Tigo Pesa Masterpa zitakazonunuliwa k wa Tigo Pesa Maste zitagharimu Sh 5,0 ya Sh 7,000 kwa wa pesa taslimu.

“Wateja wanapas *150*01# na kucha

ezo,” alisema

e, Mkuu wa wa Tigo, sema: “Tigo bwa la bei kwa Tigo Fiesta iwa kupitia ss QR. Tiketi wa mfumo rpass QR 00 pekee badala takaonunua kwa huduma) kisha kuchagua namba 2 (lipa Masterpass QR) na kutuma kiasi husika kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.”

Mpinga aliongeza: “Wateja wa Tigo pia watapata faida zaidi kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo Trivia linalotoa zawadi za kila siku za Sh 100,000, zawadi za kila wiki za Sh milioni moja, simu janja za mkononi zenye thamani ya Sh 500,000 kila moja, pamoja na donge nono la Sh milioni 10 kwa mshindi wa jumla.

LULU DIVA STAMINA ROMA

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.