Kipande ngoma ya kutambikia maharusi

Bingwa - - IJUMAA SPESHO -

KIPANDE ni ngoma ya kabila la Wasandawe ambayo inachezwa kipindi cha sherehe, hasa za jadi na harusi. Uchezaji wa ngoma hii ni wa kuruka na kutikisa mabega wakiwa katika mduara, huku wapigaji wakiwa katikati.

Wakati ngoma hiyo ikiendelea, maharusi na vijana waliotoka jando wanatolewa na kuwekwa katikati, huku wakizungukwa na wachezaji ambao midomoni mwao wanakuwa na pombe ya mtama wanafanya kama kuwatemea miguuni ili kuwatambikia.

Inapopigwa ngoma hii chakula kinakuwa ni ugali wa uwele unaoliwa na mlenda uitwao kansaa na nyama pori, kama itakosekana, basi badala yake ni mbuzi au kondoo, huku wakishushia pombe ya mtama.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.