Mwanisenga ashangazwa

Bingwa - - IJUMAA SPESHO -

NA MWANDISHI WETU

SIKU chache baada ya kuachia albamu yake ya kwanza Msikilize Mungu, mwimbaji wa Gospo anayefanya vyema jijini Mbeya, Daudi Mwanisenga, amesema anashangazwa na mapokezi makubwa aliyoyapata.

Akizungumza na Papaso la Burudani, Daudi alisema licha ya kuwa mchanga katika tasnia hiyo, albamu hiyo imeonyesha kuwa Mungu akiamua kutenda jambo hakuna anayeweza kupinga.

“Juzi nimetoa video ya wimbo Msikilize Mungu ambayo ipo katika albamu yangu ya kwanza ambayo kiukweli imenishangaza kwa kupokewa vizuri tofauti na nilivyotarajia ndani na nje ya Mbeya,” alisema David.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.