Neymar, Rabiot wazichonganisha...

Bingwa - - HADITHI -

PARIS, Ufaransa

KLABU za Barcelona na PSG, uhusiano wao unazidi kuwa mashakani, baada ya mabingwa hao wa Ufaransa kushindwa kumpeleka mwakilishi wao katika moja ya shughuli za michezo zitakazofanyika Uwanja wa Nou Camp mwezi ujao.

Shughuli hiyo maalumu hukutanisha viongozi wa klabu, shirikisho, ligi na wadhamini mbalimbali, ili kujadili maendeleo ya biashara.

Lakini kwa hali ya sintofahamu iliyopo kati ya Barcelona na PSG, imezua hofu kubwa katika siku za hivi karibuni, huku ikibainika klabu hiyo ya Ufaransa haitampeleka mwakilishi wao, Adrien Tarascon.

Ni siasa za soka kwa timu hizo zenye historia kubwa katika mchezo huo barani Ulaya, lakini kwa hivi karibuni imekuwa ngumu kuangalia hata usoni kwa mambo yanayoendelea.

Ilianza mwaka 2017, katika usajili, Barcelona walifanya mawasiliano na Marco Verratti kumshawishi ajiunge nao, huku PSG wakiwazidi kete kwa kumsajili Neymar kutoka kwa mabingwa hao wa Hispania na kuzua vita kali kati ya timu hizo.

Barcelona walishindwa kukataa kiasi cha pauni milioni 200 zilizowekwa na PSG, ambao waliwanyima Verratti, aliyehusishwa katika usajili huo wa Neymar.

Walichokifanya Barcelona ni kufungua kesi ya uchunguzi katika Shirikisho la Soka la Ulaya, ambalo halikuona tatizo lolote kwa PSG ya Ufaransa mwaka 2017.

Hivi sasa mabingwa hao wa Hispania wapo katika ushawishi mkubwa wa kutaka kumsajili kiungo wa PSG, Adrien Rabiot, ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu.

Lakini inaonekana PSG wapo tayari kumuuza kiungo huyo timu tofauti na Barcelona, ambayo mwaka jana walifanya ushawishi mkubwa wa kumng’oa Verratti ndani ya kikosi cha matajiri hao wa Ufaransa.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.