PAUL POGBA AKIRI KUSHUKA KIWANGO MAN UNITED

Bingwa - - MBELE -

KIUNGO wa timu ya Taifa ya Ufaransa na Manchester United, Paul Pogba, amekubali kuwa tangu ashinde Kombe la Dunia hajafanikiwa kucheza katika kiwango cha juu kama ilivyokuwa zamani.

Pogba hivi karibuni aliingia katika vita ya maneno na kocha wake, Jose Mourinho, ambaye alimvua kitambaa cha unahodha cha Manchester United, baada ya kuongea juu ya mwenendo wa timu kwenye vyombo vya habari.

Hivi karibuni alikubali kuwa yupo katika wakati mgumu wa kurudi kwenye kiwango chake cha siku zote.

“Ni ngumu kuanza upya, lakini najitahidi kila ninapokuwa uwanjani kuonyesha kiwango cha juu.

“Tangu nishinde Kombe la Dunia nimekuwa na wakati mgumu, japo hivi karibuni nimeanza kuwa sawa,” alisema Pogba.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.