ROSE, MCCARTHY WAACHWA ENGLAND

Bingwa - - MAKALA/HABARI -

BEKI wa kushoto wa timu ya Tottenham, Danny Rose na mlinda mlango wa Southampton, Alex McCarthy, wameondolewa katika timu ya taifa ya England kutokana na majeraha yanayowakabili.

Wawili hao walirejea katika klabu zao kabla ya kikosi hicho cha kocha, Gareth Southgate, kukwea pipa kuifuata Croatia, katika mchezo wao utakaochezwa leo.

Kuondolewa kwa Rose ni fursa kwa beki mwingine wa kushoto anayekipiga katika klabu ya Leicester, Ben Chilwell ambaye aliitwa kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Luke Shaw wa Man Utd.

Majeraha hayo yamekuja katika wakati ambao Rose ndio anarudi kwenye kiwango chake. Ikumbukwe beki huyo alianza katika mechi mbili za hatua ya makundi Kombe la Dunia mwaka huu na ile ya kusaka mshindi wa tatu dhidi ya Ubelgiji.

Aidha, licha ya kumwondoa kikosini kipa McCarthy, bado kocha wa England, Southgate, ana walinda milango watatu, Marcus Bettinelli wa Fulham, Jack Butland, anayekipiga Stoke pamoja na kipa wa Everton, Jordan Pickford.

Danny Rose

Alex McCarthy

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.