MO DEWJI ANAVYOPENDA ‘KU-TWEET’

Bingwa - - MAKALA -

HAIPITI siku bila mfanyabiashara na bilionea, Mohammed Dewji maarufu Mo, kuandika kitu katika mtandao wake wa kijamii iwe ni kwenye kurasa zake za Twitter au Instagram. Haishangazi kwa umaarufu alionao Mo, hata kurasa yake ya Twitter tayari imeshathibitishwa (verified).

Hiki ndicho alichokiandika mara ya mwisho katika ukurasa wake wa Twitter kwa lugha ya Kiingereza juzi Oktoba 10 saa 10:22 alfajiri: ‘Why aren’t schools teaching students how to do taxes and personal budgeting? (Kwanini shule hazifundishi wanafunzi masuala ya kodi na bajeti binafsi?)’

Wapenda michezo hususan mchezo wa soka, jana asubuhi waliamka kwa habari za kushtusha zilizodai kutekwa kwa Mo na watu wasiojulikana ambao walikuwa na silaha za moto. Tukio hilo lilitokea katika Hoteli ya Colloseum jijini Dar es Salaam wakati mfanyabiashara huyo akiingia ‘gym’ kufanya mazoezi.

Ni tukio ambalo baadaye lilithibitishwa kutokea na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, ambaye aliahidi Jeshi la Polisi kufanya kila liwezalo kuwatia nguvuni wahusika.

Mo licha na shughuli zake za biashara na hata wakati fulani kuwa mbunge, ni mtu anayependa michezo hususan soka, hivyo basi taarifa za kutekwa kwake ziliibua mijadala kila kona na hata kwenye mitandao ya kijamii.

Ni hii mitandao ya kijamii ambayo Mo amekuwa akiitumia kufikisha ujumbe na wakati mwingine kuweka utani. Mapenzi yake kwa mabingwa wa Ligi Kuu Bara, Simba, humfanya kuandika maneno ya utani kwenye mtandao wake wa kijamii na wale wanaosoma kuanza kuchangia. Aidha, Mo, amekuwa akiweka michoro ya vibonzo ambayo hutoka gazetini na bado watu wakajadili katika mrengo wa kiutani.

MSTARI WA JUU: Baadhi ya 'tweet' za MO Dewji. CHINI: Wanamichezo wakionyesha kwa maandiko yao mitandaoni kushutushwa na tukio la MO Dewji kutekwa

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.