FEDERER

AMPONGEZA ALIYEMNG’OA SHANGHAI MASTERS

Bingwa - - HABARI -

LICHA ya kushinda kwa seti 6-4 4-6 6-4 dhidi ya Daniil Medvedev, staa wa mchezo wa gofu, Roger Federer, amemmwagia sifa mpinzani wake huyo akisema alikuwa mwiba mchungu kwake.

Federer, mwenye umri wa miaka 37, alishinda juzi ikiwa ni mara yake ya kwanza kucheza michuano mikubwa tangu alipoishia raundi ya nne ya US Open.

"Mchezo ulionesha ni kwa kiasi gani kila mmoja alikuwa kwenye ubora na mwishowe ni maajabu kidogo tu yaliyobadilisha mambo,” alisema Federer.

Baada ya ushindi huo, sasa Federer ataisaka raundi ya tatu kwa kumenyana na nyota wa kimataifa wa Hispania, Roberto Bautista Agut.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.