Bolt rasmi kikosi cha kwanza leo?

Bingwa - - HABARI -

KUNA uwezekano mkubwa wa Usain Bolt kucheza mechi yake ya kwanza ya soka leo wakati timu yake ya Central Coast Mariners itakaposhuka dimbani kuvaana na Macarthur South West United.

Hiyo ni kwa mujibu wa kocha wake, Mike Mulvey, ambaye hata hivyo, alisema mtanange huo utakuwa wa kirafiki.

Akilizungumzia hilo, Bolt, ambaye ni mshindi mara nane wa michuano ya Olimpiki, alisema: “Kwangu, hiyo ni hatua nzuri, kocha anaporidhishwa na uwezo wako na kukuweka kikosi cha kwanza, ni hatua kubwa,” alisema Bolt juzi.

Mechi yake ya kwanza akiwa na kikosi hicho ni ile ya mwishoni mwa Agosti, mwaka huu, alipotokea benchi zikiwa zimebaki dakika 20.

Bolt anasema anaona ameimarika kwa kiasi kikubwa nafasi katika mchezo huo ambao alicheza eneo la winga wa kushoto.tangu alipopata

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.