KICHAPO CHAMVURUGA KOCHA LIVERPOOL

Bingwa - - MBELE -

KUPOTEZA mchezo wa juzi usiku dhidi ya Red Star Belgrade kumemfanya kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp, ashindwe kujua tatizo lililosababisha matokeo hayo.

Mchezo huo wa Kundi C ulimshuhudia Milan Pavkov akifunga mabao yote ya Waserbia hao, ukiwa ni ushindi wao wa kwanza msimu huu wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mechi hiyo waliyokuwa ugenini, Klopp aligusia kwa mbali uzembe uliofanywa na straika Daniel Sturridge, ambaye alikosa mabao mengi ya wazi.

Mchezaji huyo hakuwa kwenye ubora wake wa kuzipasia nyavu, hasa kipindi cha kwanza, ambapo mipira yake miwili iligonga mwamba.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.