Ishu nzima ya Ali Kiba na Wasafi Festival hii hapa

Bingwa - - MBELE - NA MWANDISHI WETU

BAADA ya uongozi wa kampuni ya Wasafi Media inayomilikiwa na msanii, Diamond Platnumz, kutangaza nia ya kushirikiana na hasimu wake, Ali Kiba, katika Tamasha la Wasafi linalotarajiwa kuanza Novemba 24, mwaka huu, staa huyo amesema yupo tayari kuwa mdhamini kupitia kinywaji chake cha Mofaya.

Hatua hiyo imekuja baada ya Ali Kiba ambaye pia ni mdhamini wa klabu ya Coastal Union ya Tanga, kuweka wazi kuwa hataweza kutumbuiza katika jukwaa la ‘Wasafi Festival’ kutokana na majukumu ya kuzindua kinywaji chake katika nchi nyingine.

“Ndugu zangu Wasafi tumepata salamu zenu, nashukuru kwa mwaliko ila kwa bahati mbaya sitaweza kushiriki kwa sasa kutokana na majukumu ya kuzindua Mofaya katika nchi nyingine. Hata hivyo, tusingependa kuwaacha hivi hivi, tupo tayari kuwapa sapoti ya kudhamini tamasha lenu ili kuweza kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya sanaa yetu Tanzania na Afrika,” alisema Ali Kiba.

Aidha, Diamond Platnumz alikubaliana na ombi la Ali Kiba na kumwagiza meneja wake, Sallam Sk, kuwasiliana haraka na meneja wa King Kiba (Seven Mosha), ili mpango huo wa udhamini ufanikiwe.

MeMo

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.