Benchi lamchosha Dida Simba

Bingwa - - HABARI - NA ZAINAB IDDY

MLINDA mlango namba mbili wa Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’, ameonekana kuchoshwa na benchi ndani ya kikosi cha kocha Patrick Asseums, jambo linalomfanya azidishe mazoezi huku akiapa kuwa siku akiaminika hataweza kufanya makosa.

Dida ambaye amewahi kuitumikia Simba kabla ya kwenda Yanga, amerejea tena kwa Wekundu wa Msimbazi msimu huu kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Pretoria University inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Afrika Kusini.

Tangu arejee Msimbazi, Dida amepata nafasi ya kukaa langoni mara moja kwenye mechi za kirafiki na mashindano ya Kagame, lakini kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara lango la timu hiyo limekuwa likilindwa na Aishi Manula.

Akizungumza na BINGWA jana, Dida, alisema kwa sasa Aishi anaongoza mapambano ndani ya Simba kutokana na kiwango chake bora, hivyo hana budi kujituma mazoezini ili aweze kupata nafasi.

“Mchezaji mzuri ni yule anayejua ubora na mapungufu yake, ndio maana nipo tayari kuendelea kujifunza kutoka kwa wale wanaopata nafasi, hata kama nimetangulia kuanza kucheza mpira.

“Hivi sasa napambana kuhakikisha napata namba kwa kufanya mazoezi nje na ndani ya timu, lengo ni kuondokana na kukaa benchi ambalo tayari limenichosha,” alisema.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.