Dante ataja udhaifu wa Lesotho, ubora Stars

Bingwa - - HABARI - NA WINFRIDA MTOI

BEKI wa Yanga, Andrew Vincent ‘Dante’, amesema timu ya Taifa ya Tanzania ina nafasi kubwa ya kupata ushindi dhidi ya Lesotho kutokana na ubora wa wachezaji waliopo na benchi la ufundi.

Stars inatarajia kucheza na Lesotho Novemba 18, mwaka huu katika mchezo wa kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Mataifa Afrika (Afcon) zitakazochezwa mwakani nchini Cameroon.

Akizungumza na BINGWA hivi karibuni, Dante, alisema alikuwepo katika kikosi cha Stars kilichocheza na Lesotho mwaka jana na kutoka sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, hivyo anajua ubora na udhaifu wa timu hiyo.

Alisema licha ya kutoka sare mchezo uliopita, kipindi hiki Stars imebadilika na inacheza soka lenye ubora tofauti na nyuma, hali inayochangiwa na kuelewana kwa wachezaji.

“Lesotho kule ninatarajia ushindi tu, umeona mwalimu ameita wachezaji mapema na wameingia kambini, watafanya mazoezi ya kutosha kwa muda mrefu tofauti na kipindi kile na ukiangalia matokeo yaliyopita kwa timu zote sisi tumefanya vizuri,” alisema Dante.

Kikosi cha Taifa Stars kwa sasa kimeweka kambi nchini Afrika Kusini chini ya kocha Mnigeria, Emmanuel Amunike, kwa ajili ya kujiandaa na mechi hiyo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.