Kocha Mtibwa atambia hazina ya wachezaji

Bingwa - - MAONI MTAZAMO KATUNI - NA DAMIAN MASYENENE, MWANZA

LICHA ya kupoteza mchezo wa juzi dhidi ya Alliance FC katika Ligi Kuu Tanzania Bara, kocha wa Mtibwa Sugar, Zubery Katwila, amesema timu yake ina hazina ya wachezaji wa kutosha watakaosaidia katika michuano mbalimbali ikiwamo ya kimataifa.

Mtibwa Sugar ilikubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Alliance FC kwenye Uwanja wa Nyamagana, Mwanza, huku bao pekee likifungwa na Dickson Ambundo, katika dakika ya 54.

Kikosi hicho kinatarajia kuiwakilisha nchi katika michuano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho barani Afrika itakayoanza Desemba mwaka huu.

Akizungumzia kuhusu kikosi hicho, Katwila, alisema hawezi kuwalaumu wachezaji kwa kupoteza mchezo kwa sababu kufungwa si tatizo.

Aidha, aliweka wazi kwamba katika dirisha dogo hatasajili kwa kukurupuka bali atasajili kulingana na mahitaji ya timu kwa kuwa anaamini kikosi chake kina hazina ya wachezaji wengi.

Hata hivyo, Katwila, alieleza kwamba wachezaji vijana waliopo kikosini hapo watatosha kuisaidia timu hiyo katika Ligi Kuu na michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

"Siwezi kuwalaumu wachezaji kwa kufungwa leo (juzi), wamecheza kadiri walivyojiandaa ila tatizo lilikuwa kwenye umakini wa kutumia nafasi.

"Hatuna muda wa kutosha kujiandaa kwa ajili ya mechi na kufanya marekebisho kwenye kikosi, pia usajili wetu utategemea na mahitaji ya timu,” alisema Katwila.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.