ZFA yafungia waamuzi wawili

Bingwa - - MAONI MTAZAMO KATUNI - NA IBRAHIM MAKAEMZANZIBAR

CHAMA cha Soka Zanzibar (ZFA), kimewafungia mwezi mmoja waamuzi wawili waliochezesha mchezo namba 43 wa Ligi Kuu visiwani humo, ambao ulizikutanisha timu za Jang'ombe Boys dhidi ya KMKM Jumapili iliyopita.

Waamuzi hao, Ali Ramadhan Ibada ‘Kibo’, aliyekuwa mwamuzi wa kati na msaidizi wake, Mustafa Hasira, wamefungiwa kutokana na kushindwa kutafsiri vyema sheria 17 za soka.

Inaelezwa walishindwa sheria namba 11 ya kuotea ‘offside’ katika mchezo huo uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Amaan, ambapo timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.

Kwa mujibu wa msemaji wa ZFA, Abubakar Khatib Kisandu, waamuzi hao wamewafungia mwezi mmoja huku wengine wakipewa onyo kali.

Adhabu ya kufungiwa kwa waamuzi itaanza Novemba 6 hadi Desemba 5, mwaka huu kwa mujibu wa kanuni ya 15(9) (e) ya ZFA.

Aidha, Kisandu, alisema ZFA haitamfumbia macho mwamuzi yeyote atakayekwenda kinyume na kanuni na taratibu za soka zinavyotaka.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.