Mabao 200 yampa jeuri Benzema

Bingwa - - SPORTS - MADRID, Hispania

FOWADIwa Real Madrid, Karim Benzema, ametamba kuendeleza moto baada ya juzi usiku kufikisha mabao 201 tangu alipotua klabuni hapo.

Benzema (30) alifunga mara mbili wakati Madrid ikiibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Viktoria Plzen katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya. "Nacheza soka ili niandike historia lakini watu huwa hawaelewi kile ninachokifanya uwanjani," alisema Benzema katika mahojiano yake na tovuti ya Madrid. "Kuna kipindi nafunga na wakati mwingine nashindwa kufanya hivyo, lakini cha msingi ni timu kunyakua taji,” alisema Benzema ambaye sasa amefikisha mabao tisa katika mechi 17 alizocheza msimu huu.

"Kuna kipindi nafunga na wakati mwingine nashindwa kufanya hivyo, lakini cha msingi ni timu kunyakua taji,” alisema Benzema ambaye sasa amefikisha mabao tisa katika mechi 17 alizocheza msimu huu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.