Aunty Ezekiel, Steve Nyerere wamwandalia dua DIAMOND

Bingwa - - IJUMAA SPESHO - NA KYALAA SEHEYE

WAIGIZAJI nyota nchini, Aunty Ezekiel na Steven Mengere ‘Steve Nyerere’, wamesema kabla ya kuanza kwa tamasha la Wasafi, wanataka kuandaaa dua maalumu kwa ajili ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Wasafi Media, Diamond Platnumz.

Hatua hiyo imekuja baada ya Diamond Platnumz kuwapa nafasi wasanii wa filamu kushiriki katika Tamasha la Wasafi, litakaloanza Novemba 24 mwaka huu, mkoani Mtwara, jambo ambalo limeonyesha uzalendo.

“Kiukweli shukrani tumempa, ila kubwa kabisa tunajipanga kufanya dua kubwa ya kumlinda na kuilinda shoo yetu, kwani Diamond ameonyesha uzalendo wa hali ya juu, sehemu ambazo ‘Festival’ hii itafanyika kuna mashabiki wengi wa filamu, hivyo watafurahi mno watakapotuona tukiwa sambamba na wanamuziki,” alisema Steve Nyerere.

Naye Aunty Ezekiel aliongeza kwa kusema kuwa: “Filamu na muziki ni vitu vinavyotegemeana, mashabiki huja kwa wingi mno pale watakaposikia mastaa wa muziki na filamu watakuwepo kwenye shoo na hili Diamond ndiye mwandaaji wa kwanza aliyeliona, haijawahi kutokea hapa nchini, tunamshukuru na tutahakikisha dua ya kumkinga na wabaya wake inafanyika ili mambo yaende sawa.”

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.