Sehzade Mahmet anachomwa mshale mgongoni mbele ya Mustafa

Bingwa - - TAMTHILIA -

MPENZI msomaji wa safu hii ya tamthilia ya Sultan, Alhamisi ya leo tunaendelea na simulizi yetu tamu na yenye mvuto mno. Ilipoishia… Kwenye gazeti la Bingwa la jana tuliona mambo mengi yakijitokeza likiwemo Feruze kutekwa.

Endelea Leo tumwangalie Ibrahim Pasha anarudi nyumbani kwake akiwa amejaa hasira, anaingia ndani anamkuta mkewe, Hadija Sultana, akiwa amesimama pembeni huku mtoto wa Niger Khalfa na Ibrahim Pasha akiwa kwenye kochi. Baada ya kutekwa, Feruze anaota kama analazimishwa anywe sumu aliyoelezwa na Hurrem anaposhtuka na kuangalia nje anagundua kwamba ametekwa. Ibrahim Pasha anatumia muda mwingi kucheza na binti yake bila kujali kuathiri mapenzi yake kwa mke na watoto wake wengine. Mkewe ambaye ni Hadija Sultana, anakasirika kumwona Ibrahim Pasha akijisahau kupenda familia yake anaona kama anawatenga watoto wengine baada ya ujio wa watoto wake wengine. NasieEfend anamtembelea Ibrahim Pasha anamkuta akiwa na binti yake wakifurahia ukaribu wao. Hurrem anapatwa na butwaa anapomwona Feruze mbele yake, anashangaa amewezaje kutoka nje ya eneo alilokuwa amemficha.

Anakumbuka namna alivyojinasua kwenye maficho hayo ni kwamba NasiEfend amefika na kumwokoa Feruze.

Feruze anamaliza mazungumzo na Hurrem kisha anaondoka anawaacha Hurrem na Sumbula wakishangazwa naye.

Hurrem anamweleza Sumbula kwamba aliyemwokoa Feruze ni Ibrahim Pasha.

Feruze anakutana na Sultan anamweleza hofu yake juu ya kifo, anamweleza mengi, Sultan anamkumbatia na kumwondoa hofu.

Tukirudi kwa wahalifu wawili waliookolewa na Sehzade Mustafa, wanafanya vurugu kwenye kasri la Mustafa wanafikishwa kwa Mahdevran.

Naye kiongozi wa jeshi la maji anafika na kuzungumza na Sultan Suleiman, hayo yakiendelea Hurrem anazungumza na Rostima anampa maagizo mapya kuhusu cha kumfanyia Feruze.

Sehzade Mustafa anaamshwa anakutana na Helena, wanazungumza huku Ibrahim Pasha akikutana na jaji mkuu wa Ottoman wanazungumza lakini hawafikii mwafaka.

Sultan na familia yake akiwemo Hurrem, Sehzade Meemet, wanamtembelea Sehzade Mustafa kwenye jimbo lake.

Sultan anamjalia Baraka mjukuu wake anampa jina Suleiman ingawa Hurrem anakasirishwa na hayo.

Ibrahim Pasha na Hadija Sultana wanagombana wanarushiana maneno machafu, Ibrahim Pasha anaamua kuondoka kuepusha ugomvi zaidi.

Mihrimah anakutana na mwanamume anayempenda baada ya matembezi jimboni kwa Sehzad Mustafa anamkabidhi kitabu chake cha mashairi kisha anaondoka kwa aibu maana alichofikiria kuelezwa hajaelezwa licha ya kuonyesha dalili za kumpenda.

Feruze Hatum anakutana na Hafidha Hatum na Rostima anakaribishwa kwenye farasi lakini Hafidha Hatuma anamwonya kwa anachokifurahia anamweleza ni hatari kubwa.

Pasha anaendelea kufurahia maisha na binti yake. Rostima anamkabidhi Feruze farasi lakini hata hivyo hampandi.

Sultan anakwenda sokoni na wapambe wake pamoja na watoto wake anapokea maoni ya wafanyabiashara mbalimbali lakini kwa mbali kuna mtu anawafuatilia.

Lakini yule anayemfuatilia ni yule mfanyabiashara aliyeporwa mpenzi na Helena, anakamatwa na watu wa karibu wa Sehzad, lakini anafanikiwa kusema mambo mengi aliyofanyiwa na Mustafa.

Hurrem anazungumza na Helena anamwelekeza mambo mengi ya namna ya kuishi katika jumba hilo na namna ya kuwa mwanamke mwenye heshima huku akimuonya mambo kadhaa kama anataka kuheshimika.

Wanaporudi kwenye jimbo la Sehzad Mustafa, Sultan anamsema sana Sehzad Mustafa kwa mambo yote aliyosikia walipokuwa sokoni.

Anamweleza anamtaka atende mema kwa watu wake na si kulazimisha mambo au kuwatesa watu wanaomzunguka.

Sultan Suleiman anakasirishwa na anayoyakuta katika jimbo hilo anataka warudi walipotoka kama hawawezi kuishi hapo na kuwatumikia watu wake.

Muda mrefu anaoutumia Sultan Suleiman kuzungumza na Sehzade Mahmet, kunamkwaza Sehzade Mustafa, anahisi upendeleo kwa Mahmet kutoka kwa baba yao ambaye ni Sultan.

Sultana Mihrima na mwandishi wa mashairi wanakutana wanazungumza kimapenzi, lakini mazingira yanamkwaza Mihrima anashindwa cha kufanya anachotaka kufanya mwanaume mwandishi mahiri wa mashairi kipenzi chake mkubwa.

Nigar Kalfa na Rostima wakiwa ndani bado maneno ya Hurrem yanamuumiza Rostima kwamba awe makini na Niger Khalfa licha ya Niger kuonyesha kumpenda Rostima.

Hadija anajaribu kumtuliza Ibrahim Pasha, Pasha anatulia wanarudisha mapenzi yao.Wakati hayo yakitokea, Niger Khalfa anamwogesha Rostima lakini Rostima anagoma anamtaka Niger aache kumuogesha kwamba ataoga mwenyewe, Niger anaondoka Rostima anaoga mwenyewe akiwa katika mawazo mengi ya nini afanye.

Wakati Niger akiwa katika mawazo ya kimapenzi kwa Rostima, anasikia mlango ukigongwa anapofungua anakutana na NasiuEfend, wanaongea mengi kuhusu maisha yake pamoja na Pasha.

Rostima anampa farasi Feruze lakini anamfungua kamba ili adondoke na kweli anadondoka Rostima anamfuata Feruze ili amuue lakini anapojaribu kufanya hivyo anaona alama ya muhuri inayomkumbusha kitu anashindwa kumuua anamwacha.

NasieEfend anamchukua Niger Khalfa na binti yake hadi kwenye nyumba moja huko nje ya mji wa Ottoman.

Sehzade Mahmet na Mustafa wanazungumza huku wazazi wao Mahdervan na Hurrem nao wakizungumza yao hasa majigambo baina yao hadi Sultan anapofika kwenye eneo lao.

Mustafa na Mahmet wanapokuwa katika mazungumzo, Mahmet anaonekana kutofurahishwa jambo anamweleza kaka yake Mustafa anamtuliza lakini anapopiga hatua kuondoka ghafla Mahmet anapigwa mshale wa sumu anadondoka mbele ya Mustafa.

Je, nani amerusha mshale huo kwa Mahmet, nini atasema Hurrem, Sultan watakapopata taarifa kwamba Mahmet amechomwa mshale. Usikose kufuatilia simulizi hii kesho maoni na ushauri 0755-625042.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.