ED WOODWARD AMPA TANO MOURINHO

Bingwa - - MBELE - LONDO, England

KOCHA Jose Mourinho, jana alipata pongezi nyingi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Manchester United, Ed Woodward, baada ya kuiwezesha timu hiyo kuondoka na ushindi dhidi ya Juventus katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kabla ya kupata ushindi huo, awali walionekana wangeambulia kichapo baada ya nyota wao wa zamani, Cristiano Ronaldo, kupachika bao ambalo liliwafanya vinara hao wa soka Italia waongoze. Hata hivyo, mpira wa adhabu uliopigwa na Juan Mata, dakika ya 86 na lile la kujifunga la Alex Sandro, zikiwa ni dakika za mwisho cha mchezo huo ndilo likawafanya waondoke uwanjani wakiwa kifua mbele. Pamoja na ushindi mastaa wa timu hiyo hawakuweza kusherehekea mjini Turin kufuatia Jumapili wanakabiliwa na mechi ngumu dhidi ya Manchester City na hivyo mapema jana wakatua nchini England. Mourinho na vijana wake walitua nchini England jana saa 10:30 alfajiri na kupokelewa na mkurugenzi huyo ambaye alionekana kumpongeza sana Mreno huyo. Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, wawili hao walionekana wakimwaga tabasamu baada ya kukutana na huku wachezaji wakipita mbele ya kamera.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.