TANO KALI

Bingwa - - SPORTS -

Imetosha

Filamu ya Imetosha ambayo imechezwa na Vicent Kigosi ‘Ray’, Kajala Masanja na Cassie Kabwite, imeanza kuonekana tangu Novemba 3, mwaka huu. Imechezwa nchini Zambia, mhusika mkuu akiwa Ray ambaye alienda Zambia kucheza soka, jambo linalofanya filamu hiyo iliyotengenezwa kwa kiwango cha hali ya juu kuwa ya kuvutia na kutazamwa na mashabiki wengi.

Day After Death (D.A.D)

Hii ni filamu ni ya mapenzi inayohusisha mastaa wawili mmoja kutoka Ghana, Van Vicker na Wema Sepetu wa Tanzania. D.A.D ambayo imechezwa kwenye nchini mbili ilianza kuonyeshwa katika mtandao wa MPTV tangu mwezi uliopita na kupata watazamaji wengi kuliko filamu zote zilizowekwa na mtandao huo.

Nipe Changu

FILAMU ya Nipe Changu ambayo imecheza na Daud Michael 'Duma' inatarajiwa kuzinduliwa kesho Agosti 18, mwaka kwenye Ukumbi wa Mlimani City Century kwa kiingilio cha shilingi 50,000.

KAFARA

Filamu hii inahusu ukame, njaa, misukosuko na kila aina ya tabu inatokea katika kijiji cha Bumbulu. Wanakijiji wanakumbushwa kutoa kafara ili mambo yaende sawa na Mwajabu, ambaye ni binti pekee kwa mama yake anachaguliwa kutolewa kafara, hapo ndipo hekaheka inaanza.

MWALI WA UJI

Filamu hii ambayo ilitoka Jumatatu iliyopita, inamhusu msichana (Hairuni), aliyeolewa na mwanamume ambaye wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani anamfanyia fujo kwa kutofuata misingi ya funga hiyo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.