NA WINFRIDA MTOI

Bingwa - - IJUMAA SPESHO -

MAGONGO

LIGI ya mpira wa magongo kwa shule za msingi na sekondari, Mkoa wa Dar es Salaam, inatarajia kuendelea wikiendi hii kwenye viwanja vya JMK Youth Park, ikiwa ni hatua ya pili ya michuano hiyo.

Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Magongo Mkoa wa Dar es Salaam (DRHA), Mnonda Magani, alisema ligi hiyo ilianza wiki iliyopita na inatarajia kumalizika Aprili, mwakani.

KABADDI

WACHEZAJI wa timu ya taifa ya mchezo wa kabaddi Tanzania, wanatarajia kucheza michezo ya kujipima wenyewe kwa wenyewe kesho, kwenye viwanja vya JMK Youth Park kujiandaa na michuano ya Afrika Cup.

Mwenyekiti wa Kabaddi Tanzania, Abdallah Nyoni, amesema Novemba 21, watafanya mchujo kuchagua wachezaji watakaokwenda Kenya katika mashindano hayo, Desemba, mwaka huu.

NGUMI

TIMU ya ngumi ya klabu ya urafiki jijini Dar es Salaam, wikiendi hii inaendelea kujifua kwenye Uwanja wa Kinesi, Sinza, kujiandaa na mashindano ya Klabu Bingwa Mkoa.

Kocha wa timu hiyo, Sudi Ally, alisema wana mabondia wa wanawake na wanaume wenye uwezo mkubwa, hivyo kutokana na ukongwe wa klabu hiyo wanachohitaji ni kutwaa ubingwa huo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.