Coutinho kusugua benchi wiki tatu

Bingwa - - SPORTS -

MADRID, Hispania

KLABU ya Barcelona imethibitisha kuwa nyota wake, Philippe Coutinho, huenda akakaa nje ya uwanja kwa muda wa zaidi ya wiki tatu kufuatia matatizo ya misuli yanayomkabili.

Nyota huyo wa timu ya Taifa ya Brazil, alicheza dakika zote 90 za mcheo huo ambao Barca walitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Inter Milan katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini alikuwa hajisikii vizuri.

Taarifa iliyotolewa jana na klabu hiyo ilieleza kuwa vipimo alivyofanyiwa jana staa huyo vinaonesha kuwa ana mpasuko kidogo kwenye msuli wake wa nyama za paja za mguu wa kushoto.

"Kwa tatizo hilo anaweza kuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya wiki tatu,” ilieleza taarifa hiyo.

Kwa majeraha hayo sasa Coutinho atazikosa mechi za mwishoni mwa wiki ikiwamo dhidi ya Real Betis katika michuano ya La Liga na za Brazil za kirafiki zitakazofanyika nchini England dhidi ya Uruguay na Cameroon.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.