WENYE BUKU 7 RUKSA TAIFA, NKONGO KATI

BURUDANI - - MBELE - NA NASRA KITANA

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetangaza viingilio ya mechi ya ligi kuu ya Tanzania Bara kati ya Yanga na Simba ambapo kiingilio cha chini ni sh. 7,000.

Mchezo huo ambao ni wa raundi ya nne unatarajia kuchezwa Jumamosi hii katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mechi itaanza saa 10:00 jioni.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa TFF, Baraka Kizuguto alisema kiingilio cha juu katika mchezo huo kitakuwa 30,000 katika VIP A.

Alisema VIP B na C vitakuwa sh. 20,000 huku mashabiki watakaokaa viti vya bluu na kijani watalipa sh. 7,000.

Kizuguto alisema ulinzi utaimarishwa katika mchezo huo kutokana na mechi za timu hizo kuingiza mashabiki wengi.

Alisema mechi hiyo itachezeshwa na mwamuzi wa kimataifa mwenye beji ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Israel Nkongo akisaidiwa na Ferdinand Chacha kutoka Mwanza na Josephat Bulali wa Dar es Salaam.

Kizuguto alisema mwamuzi wa akiba atakuwa Soud Lila kutoka mkoa wa Pwani.

Nkongo atachezesha akiwa na kumbukumbu mbaya ya kupigwa na wachezaji wa Yanga katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam FC miaka miwili iliyopita.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.