SNOOP DOGG

BURUDANI - - MAKALA -

DUNIA ina mambo! SNOOP Dogg ameanzisha tovuti ya mfumo wa maisha ya bangi.

Rapa huyo, ambaye hafichi mapenzi yake katika matumizi ya dawa za kulevya, ameshirikiana na Ted Chung kubuni mchezo wa Merry Jane uliotawaliwa na kipengele cha bangi.

Taarifa za tovuti hiyo zitahusu bidhaa ya bangi na ramani inayoonyesha sehemu za kupata huduma.

Sehemu mojawapo itakuwa ikitoa mahojiano mfululizo ya watu wanaopenda kuvuta bangi.

Akieleza dhamira yake kuhusu tovuti hiyo, Snoop alisema: “Watu wengi sana wanakaribishwa. Tunawapa nafasi kuja karibu na kueleza wanapenda kuvuta. Mimi ni mvutaji, jina langu Snoop Dogg, ni mvutaji.

“Kwangu ni hali ya amani. Kila wakati ninapokuwa, naona vitu vizuri vinatokea. Naona watu wenye upendo, amani na ari.

“Tutakuwa kama kitabu cha kumbukumbu ya kila kitu kuhusu bangi duniani.”

Wavuta bangi maarufu Seth Rogen na mwimbaji Miley Cyrus nao wamejumuishwa kwenye tovuti hiyo.

Akitangaza mpango wake huo katika mkutano uliofanyika mjini San Francisco, Snoop alibainisha kuwa tovuti hiyo itapokea watumiaji 420 kwa siku na itazinduliwa rasmi mwezi ujao.

CALIFORNIA, MAREKANI

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.