U-17 Ilala kupongezwa

BURUDANI - - HABARI -

CHAMa cha Soka Wilaya ya Ilala (IDFA) kijipanga kuiandalia sherehe kubwa timu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17, ambayo hivi karibuni imetawazwa bingwa wa michuano ya ‘Airtel Rising Stars’.

Timu hiyo ya mkoa wa kisoka wa Ilala, imefanikiwa kutwaa kombe hilo, baada ya kuilaza mabao 4-0 timu ya mkoa wa Mbeya kwenye mechi ya fainali ya michuano hiyo iliyochezwa Jumatatu iliyopita katika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam hivi karibuni Katibu wa chama hicho, Daudi Kanuti alisema ushindi huo kwa kiasi kikubwa umeamsha ari na shauku kwa timu za wilaya hiyo wakati zitakaposhiriki michuano mingine kama hiyo.

“Ni ushindi wa kujivunia sana, kwani licha ya michuano hiyo kuwa na ushindani mkubwa, vijana wetu wamepambana vikali na hatimaye wamefanikiwa kulinda heshima yetu kwa kutwaa taji hilo msimu huu,” alisema Kanuti.

Katibu huyo, alisema baada ya kuifanyia sherehe timu hiyo, uongozi wa IDFA na wachezaji wamepanga kulipeleka kombe hilo kwa Mkurugenzi wa wilaya hiyo.

Alisema hatua hiyo ina lengo la kuwaonyesha viongozi hao ubora wa timu za vijana ulioko kwenye wilaya

MWANARIADHA mkongwe nchini, Zakia Mrisho, amesema anatamani kuiwakilisha Tanzania kwenye michezo ijayo ya Olimpiki itakayofanyika mwakani jijini, Rio de Jeneiro, Brazil kama mchezaji wa mbio ndefu.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka mkoani Arusha hivi karibuni, Zakia alisema hatua hiyo imelenga kumwezesha kufanya vyema kwenye michuano hiyo mikubwa duniani.

“Unajua tangu nilipoanza mchezo huu nimekuwa ninakimbia mbio za mita 5,000. Lakini sasa najipanga kuhama katika umbali huo, ili ikiwezekana katika Olimpiki ijayo nikimbie mita 10,000,” alisema Zakia.

Alisema kwa muda mrefu amekuwa akijifua katika mbio hizo na hali inamwendea vizuri katika mkakati huo.

Mwanariadha huyo amewasihi wanariadha wenzake na wachezaji wengine ambao wanajipanga kuiwakilisha nchi katika michuano hiyo ya Olimpiki, kuanza mazoezi mapema ili kuwawezesha kufuzu kwa kufikia viwango vizuri

vinavyohitajika.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.