Bosi Sofapaka mawazo kibao

BURUDANI - - AFRIKA - NAIROBI, KENYA

MWENYEKITI wa timu ya soka ya Sofapaka,Elly Kalekwa amesema kwamba bado ana mawazo kuboresha kikosi chake kwa ajili ya kusajili wachezaji mahiri.

Kalekwa alisema jana, wakati akizungumza na gazeti moja la nchini Kenya kwamba amepanga kufanya hivyo ili kujenga kikosi imara.

Alisema lengo lake kubwa ni kutaka kurejesha kikosi cha ushindi baada ya kugundua baadhi ya kasoro ndani ya timu hiyo kuanzia benchi la ufundi.

“Nina mpango wa kufanya mageuzi makubwa ndani ya timu hii,lakini kwanza nitaanza na kocha na benchi zima la ufundi,”alisema.

Hata hivyo,kiongozi huyo,alishindwa kuthibitisha kama anaweza kumpandisha David Ouma kuwa kocha mkuu baada ya Sam Timbe kuondoka.

“Ukweli tutamkumbuka sana Timbe,lakini hayo yote ni maisha hayawezi kuishia hapo,tunasonga mbele kwa kujipanga upya,”alisema Kalekwa.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.