Bodi ya Ligi angalieni hili

BURUDANI - - WAZO | HOJA -

M WA N A M U Z I K I Beyonce Knowles ameibuka na video yenye nyimbo mpya ya Runnin ambayo imeanza kupigwa katika vituo mbalimbali vya Luninga na redio.

Mrembo huyo ametoa kibao hicho,wiki iliyopita ambacho ameshirikiana na Naughty Boy ambacho kimeanza kutesa nchi humo.

Kazi ya kutengeneza nyimbo hiyo,imefanywa na diva and Arrow Benjamin ambapo imekuwa kivutio kwa watazamaji wa vituo vya televisheni.

Kwenye video hiyo,mrembo huyo anaonesha akifanya vitu vyake vya mahaba licha ya kutomshirikisha mumewe Jay Z. IKI iliyopita michuano ya Ligi Kuu iliendelea katika viwanja mbalimbali hapa nchini huku timu ya Toto Africa ikicheza na Coastal Union.

Mchezo huo,ulifanyika kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani,mkoani Tanga ambapo timu hizo zilitoka suluhu.

Lakini kwenye mchezo huo,kulizuka mambo ya ajabu ambapo kocha msaidizi wa timu ya Toto Africa ya Mwanza,John Tegete alitoa tuhuma nzito.

Tegete alidai kwamba kwenye chumba ambacho walikuwa wakae wachezaji wao waliwekewa dawa na kuamua kugoma kuingia.

Hakika taarifa hiyo imeweza kunishtua na kuamua kuandika ujumbe huu ili kuikumbusha bodi hiyo kama kuna ukweli wachukue hatua kali.

Kocha huyo alidai kwamba waliwekewa dawa zenye harufu kama mafuta ya manukato lakini walishtuka yanaweza kuwaathiri wachezaji wao kwenye mchezo huo.

Msimu uliopita kulikuwepo na taarifa kama hizo hasa kwenye uwanja wa CCM Kambarage na kufikia hatua kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Nchini(TFF),Boniface Wambura kwenda kuchunguza.

Hatua hiyo ilikuja baada ya baadhi ya timu kudai kwamba walipuliziwa dawa hizo kwenye vyumba vyao kitu ambacho hadi leo hakuna taarifa zaidi iliyotolewa.

Umefika wakati kwa bodi hiyo,kwa vile iko chini ya mtu mwenye uwezo mkubwa wa kufanya kazi ambaye ni Wambura nina imani atafanyia kazi na kubaini ukweli.

Ikiwa itabainika kuna ukweli basi vyema wahusika wote wachukue hatua kali dhidi yao na kuondoa tabia hiyo ambayo huenda itaota mizizi.

Lengo ni kuona ushindani kwenye michuano hiyo unazidi kufanyika ili tuweze kupaya timu imara ya Taifa, kupitia ligi hiyo.

Itakuwa ni aibu kwa nchi endapo itabainika vitendo hivyo vinafanyika na kusababisha pengine kufungiwa endapo timu kutoka nje ya nchi zikija na kubaini kuwepo jambo hilo.

Nawaomba viongozi wa TFF na bodi hiyo kuchukua tahadhari mapema ili kuzuia vitendo hivyo kuendelea kufanyika kwa vile ni hatari sana.

LOS ANGELES, Marekani

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.