Tonto Dikeh aweka msimamo

BURUDANI - - WAZO | HOJA -

SANII James Ikechukwu Esomugha maarufu kwa jina la Jim Iyke ametoboa siri kwamba ataendelea kujifunza baadhi ya vitu kutoka kwa 50 Cent ili aweze kuwa msanii bora.

Lyke alisema jana wakati akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari nchini humo kuwa amekuwa anavutiwa na kazi za mwanamuziki.

Alisema kupitia 50 Cent ameweza kufanya vitu vingi kwa vile kila kazi anayotoa msanii huyo lazima anunue ili kujifunza jambo ambalo analifanya.

“50 Cent kwangu ni mtu muhimu,navutiwa na kazi zake,pamoja na kufanya nae baadhi ya kazi,lakini bado ninaendelea kujifunza kila kukicha kupitia kwake,” alisema.

MWIGIZAJI Tonto Dikeh amesema kwamba amelazimika kufunga ndoa ya jadi ili kuwafunga mdomo maadui zake.

Mrembo huyo,alisema jana wakati akizungumza na gazeti moja la nchini humo kuwa aliamua kufunga ndoa mwishoni mwa mwezi Agosti,mwaka huu.

Alisema amefunga ndoa na Oladunni Churchill ‘Mr X’ ili kuondoa tabu aliyokuwa anaipata kutoka kwanaume waliokuwa wanamtamani kimahaba.

“Wanaume wengi walikuwa wananifuata kunitaka,sasa jamani nimefunga ndoa na Churchill,sitaki kufuatwa tena nina mume,”alisema.

Hata hivyo,mrembo huyo amesema kuwa yeye na mumewe wamefunga ndoa ya jadi kwa makubaliano kwamba aendelee na kazi zake za kuigiza.

LAGOS, NIGERIA

ABUJA, NIGERIA

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.