HAMTOKI

Kiiza: Mungu yupo

BURUDANI - - MBELE - NA NASRA KITANA

TAMBO kati ya wachezaji wa Simba na Yanga zinachochea hisia kuwa hakuna timu itakayotoka Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na matokeo ya sare, bali kulala na maumivu ya kufungwa baada ya dakika 90 za pambano hilo la watani wa jadi.

Wakizungumzia pambano hilo ambalo litachezwa keshokutwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, nahodha wa Yanga Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na mshambuliaji wa Simba Hamis Kiiza, kila mmoja ametambia timu yake.

Canavaro, akizungumza kwa kujiamini amewatumia salamu mahasimu wao kwamba hawatoki salama na watawachapa mabao mengi kwa sababu hawana jeuri ya kuhimili kasi waliyoanza nayo katika ligi kuu msimu huu.

Alisema kuwa wameanza ligi vyema kwa kila mechi kutoka na pointi tatu, hivyo hawataki rekodi hiyo ichafuliwe kwa kufungwa na Simba.

“Tumejipanga vyema kama timu tunahitaji kuwafunga Simba kwa gharama yoyote, tunafanya mazoezi kwa umakini na tutahakikisha siku hiyo lazima tuwape raha mashabiki wetu,” alisema Cannavaro.

Wakati beki huyo kisiki akiwatoa hofu wapenzi wa Yanga kwa kuwahakikishia kuwa ushindi ni wao kwa vile wamechoka kugeuzwa ‘mbuzi wa kafara wa Simba’, Kiiza amejibu mapigo namna hii:

“Nawaambia mashabiki wa Simba wasiwe na presha na mechi ya Yanga kwani ni mechi ngumu lakini hatukubali kufungwa, tutacheza kadri ya uwezo wetu.”

Kiiza mwenye usongo wa kuwaumbua Yanga kwa kuwafunga kutokana na kuwa na hasira nao ya kumtosa, amesema baada ya kusajiliwa Simba alikuwa anasubiri kwa hamu kutimiza ndoto ya kuinyoa timu hiyo.

“Ni mechi ngumu sana inafaa kujipanga zaidi, lakini tunaomba Mungu tuweze kupata matokeo mazuri kwenye mechi hiyo,” alisema Kiiza.

Alisema atakuwa mwenye furaha sana watakapoifunga Yanga kwani watathibitisha uwezo wake katika timu ya Simba.

Hata hivyo kiiza aliwataka mashabiki wa klabu yake wasiwe na wasiwasi na klabu yao kwa sababu ushindi upo pale pale kwani wamejipanga vyema.

Msimu huu timu ya Simba chini ya kocha Dylan Kerr aliyezaliwa Januari 14, 1967 na ambaye alikuwa beki kabla ya kutundika daluga, imekuwa na matokeo ya kuvutia kutofautisha na misimu miwili iliyopita ilipokuwa ikianza ligi kwa kusuasua.

Mpaka sasa timu hiyo inayoshika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi imeshinda mechi tatu na kufikisha pointi tisa sawa na Yanga, lakini inazidiwa mabao matatu ya kufunga. Zote zimeruhusu bao moja katika wavu wake.

Tayari Simba wamejichimbia Unguja na wanatarajiwa kurudi jijini, Dar es Salaam, leo au kesho kuwasubiri Yanga ambao pia wamejificha katika visiwa hivyo vya marashi ya karafuu wakiwa upande wa Pemba.

Karibu wiki nzima kocha wa Yanga,Hans van der Pluijm aliyezaliwa Januari 3, 1949 na kucheza katika nafasi ya kipa, amekuwa akijinasibu watashinda na kazi aliyokuwa anaifanya kambini katika timu yake ni kuwajenga wachezaji kisaikolojia na kuwakumbusha mabeki jukumu lao la kutengeneza ‘ukuta wa Berlin’.

MUSA Mgosi

Tambwe

AMIS

KHAMIS Kiiza

UWANJA Taifa ambako Simba na Yanga zitaumana Jumamosi .

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.