WENGER HANA MKE

BURUDANI - - MBELE -

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger ameachana rasmi na mke wake, kwa mujibu wa ripoti.

Wenger na aliyekuwa mpenzi wake wa siku nyingi Annie wameachana baada ya jaji mjini Paris kutoa hukumu hiyo ya kuwatenganisha wawili hao, hivyo kila mmoja anaweza kuwa na mpenzi mwingine.

Gazeti la The Sun la Uingereza jana liliandika kwamba, Wenger bado anatarajiwa kutoa fedha za matunzo kwa Annie.

Chanzo kimoja kililiambia gazeti hilo: “Wamekubaliana mgawanyo wa mali pamoja na fedha.

“Hawakuwa na furaha kwa muda, waliona uamuzi huo unafaa kuchukuliwa.”

Hukumu hiyo, inaeleza wenza hao waliokuwa wakiishi mbalimbali miezi kadhaa, hawajapeana talaka lakini kisheria imefafanuliwa hawatakuwa pamoja tena.

Wenger na Annie walianza kuwa na uhusiano wa mapenzi tangu katikati ya miaka ya 1990, kabla kufunga ndoa 2010. Wana mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 18 ambaye anaitwa Lea.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.